BREAKING NEWS: Roma Ajibu Kuhusu Kuonekana na Wema Sepetu Hotelini



Msanii wa muziki Bongo, Roma amefunguka kuhusu taarifa za yeye kufanya video na  Wema Sepetu.

Rapper huyo katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm amesema kuwa walikutana hotelini kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ndipo wakapiga picha na hakukuwa na zaidi ya hapo.

"Hiyo stori ya Wema nilikutana naye nilikuwa naenda Ivan (jina la hoteli) kula lunch, kwenye moja na mbili tukawa tunapiga naye stori ndiyo hizo picha zikaja lakini hamna chochote, sio mchongo wa chupa wa video, ni familia tu," amesema Roma.

Kwa sasa Roma na Stamina (Rostam) wanafanya vizuri na wimbo wao mpya uitwao Parapanda mara baada ya kufanya vizuri na ngoma kama Hivi Ama Vile pamoja na Kiba_100

Comments

Popular Posts