BREAKING NEWS: Watu 82 wafariki dunia huko Indonesia katika tetemeko la ardhi kisiwa cha Lombok

Image result for Scores killed in Indonesia island quake

Mamlaka nchini Indonesia inasema zaidi ya watu 82 wamefariki baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukipiga kisiwa cha Lombok.
Maafisa wa idara ya kudhibiti majanga wanasema mamia ya watu wamejeruhiwa vibaya kwa tukio hilo lililotokea Jumapili.
Tetemeko hilo lenye nguvu ya 7 kwenye vipimo vya Richter limeharibu vibaya miundombinu ya umeme na barabara sambamba na nyumba.
Katika kisiwa jirani cha Bali picha za video zimeonyesha watu wakikimbia majumbani mwao huku wakipiga kelele za msaada.
Tetemeko hili limekuja wiki moja baada ya jingine kuipiga sehemu hiyo ya Lombok, kisiwa maarufu kwa shughuli za utalii ambapo watu 16 waliuawa.
Hatari ya kuwepo kwa kwa kimbunga ilitangazwa kisiwani hapo lakini ikaondolewa saa chache baadae.
Msemaji wa idara ya kudhibiti majanga ya Indonesia amesema nyumba nyingi zimeathirika vibaya, ambapo nyingi kati ya hizo zilijengwa kwa kutumia nyenzo duni.


Waziri wa mambo ya ndani wa Singapore Kasiviswanathan Shanmugam alikua ziarani katika kisiwa hicho ambapo ametuma picha kwenye mitandao ya kijamii akionyesha namna chumba chake kilivyoathirika.

Comments

Popular Posts