HABARI: Azam FC inajifua kinoma Uganda








Dar es Salaam. AZAM FC inaendelea kujifua vilivyo nchini Uganda, ili wakirejea kuanza ligi Agosti 22, waanze kwa mafanikio huku malengo yao yakiwa ni kutwaa ubingwa wa ligi na Kombe la FA.
Meneja wa timu hiyo, Philip Alando alielezea maandalizi yanayoendelea nchini Uganda kwamba watacheza mechi za kirafiki na jana Ijumaa jioni walitarajia kucheza na URA wakiamini ndio kipimo sahihi cha kujua ufiti wa wachezaji wao.
"Tumeanza na URA, tutaendelea kucheza mechi za kirafiki naamini tutafanya vizuri tu na maandalizi yataenda vizuri, lengo kubwa ni kuhakikisha tunapigania ubingwa wa ligi na FA.
"Naamini jambo hilo litafanikiwa chini ya makocha wenye uwezo wa hali ya juu ambao ni Hans Pluijm, Juma Mwambusi na Idd Cheche ambao wanaendelea na kazi yao,"alisema.
Alisema kikosi kipo imara na kwamba ushindani wa namba unaonekana kwa safu zote, kulingana na usajili ambao wameufanya kwa msimu huu, wakiamini wamepata mastaa ambao ni msaada akiwemo Donald Ngoma waliyemtoa Yanga.
By OLIPA ASSA

Comments