HABARI: Wawa anatumia pesa mbaya Uturuki

Kartepe. Kati ya watu waliotumia pesa nyingi nchini Uturuki mpaka sasa ni beki wa kati, Muivory Coast Pascal Wawa.
Hii ilijionyesha siku ambayo wachezaji hao walikwenda kufanya manunuzi mjini siku ya Jumatatu.
Wawa ambaye alinunua bidhaa kama viatu, suruali aina ya jeans, tisheti na vitu vingine vingi ambavyo kwa mahesabu ya haraka ni zaidi ya dola 300 (zaidi ya shilingi laki sita).
Wachezaji wengine waliofungasha mizigo mingi ni Emmanuel Okwi raia wa Uganda, Mnyarwanda Meddie Kagere, Mzambia Cletus Chama, Adam Salamba, Deogratius Munishi 'Dida'.
Sehemu kubwa ya wachezaji hawa walinunua viatu vya aina tofauti vya kuchezea soka na matembezi.
Baadhi ya wachezaji kama Waghana Asante Kwasi na James Kotei na wengine hawakununua vitu kabisa na walidai hawakuridhika na vitu walivyoviona hapo, walidai wangefanya hivyo katika shopping yao ya mwisho Istanbul.
"Vitu vya hapa si vizuri na bei iko juu, sisi tunataka viatu vizuri vya kutokea na kuchezea mpira,"alisema Kwasi.
By Doris Maliyaga
Comments
Post a Comment