NEWS: Magufuli aeleza jinsi anavyotumia wanaotoka upinzani kama silaha

Rais John Magufuli
Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametumia hafla ya kuapishwa kwa wakuu wa mikoa, manaibu katibu wakuu na makatibu tawala wa mikoa kukumbusha majukumu yao katika maeneo ya utendaji, lakini akadokeza kuwa amekuwa akiteua waliokuwa waliokuwa upinzani kama silaha za kushambulia walikotoka.
Miongoni mwa walioapishwa leo Agosti Mosi ni mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, David Kafulila ambaye amekuwa katibu tawala wa mkoa wa Songwe, lakini orodha ya walioteuliwa juzi pia inamjumuisha wanasiasa wengine kutoka vyama vya upinzani.
Kuteuliwa kwa wanasiasa hao kutoka upinzani ni mwendelezo wa maamuzi ambayo Rais amekuwa akifanya na ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakitafsiri kuwa yanaweza kuua upinzani.
Lakini leo Agosti Mosi wakati wa kuapisha viongozi aliowateua, Rais alikuwa na maelezo ya uteuzi huo wa wanasiasa wanaotoka vyama vya upinzani.
“Wapo wengine wanasema nimechagua (wanasiasa) wa upinzani, nani ni mpinzani wa Tanzania. Sisi wote ni Watanzania,” alisema Rais Magufuli.
“Hata hivyo, ndugu zangu, mkiwa mnapigana kwenye vita, mkateka vifaru, mkateka mizinga, mkateka bunduki unakuja kuziweka kwenye stoo? Si unazigeuza kuwapigia hao hao waliopo?
“Lakini pia, hata ukiteka mateka, mabregadia jenerali, unakuja kuwaweka wawe wanakula chakula chako? Si uwarudishe huko wakawe wanapigwa ili vita ikolee vizuri ukawape na silaha?” alisema Rais Magufuli.
Kuhusu Kafulila, Rais Magufuli alieleza kuvutiwa kwake na jinsi alivyopambana katika kashfa ya uchotwaji fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow uliosababisha mawaziri na watendaji wakuu wa Serikali kulazimika kujiuzulu au kutumbuliwa.
“Ndugu yetu Kafulila alipokuwa huko kwenye chama chake alipigania suala la IPTL," alisema akizungumzia kampuni hiyo ya ufuaji umeme liyokuwa katikati ya sakata hilo la uchotwaji wa Sh306 bilioni.
"Uwe CCM, uwe Chadema uwe CUF uwe huna chama, suala la IPTL halina chama. Lakini (Kafulila) alisimama akapingwa, akaitwa tumbili akaitwa nani. Wala hajageuka kuwa tumbili, ni huyu huyu," alisema Rais.
"Huyu siyo mpianzani bali ni mtekelezaji wa ilani ya CCM.”
Alisema katika makatibu tawala aliokuwa akiwaapisha, mtu pekee aliyetokea upinzani ni Kafulila.
“Ukingalia ma-RAS, aliye-cross chama ni mmoja tu. Kafulila, katika 13 wote. Ukienda kwa Ma-DC wako 31. Niliowakuta nafikiri ni watatu na nusu walio cross vyama vingine," alisema.
Aliwataja wakuu hao wa wilaya kuwa ni Patrobas Katambi, aliyekuwa mwenyekiti wa vijana Chadema ambaye sasa anakuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Moses Machali (Nanyumbu), na Said Nkumba, ambaye alihamia Chadema na baada ya uteuzi wa wagombea kuisha, alirejea CCM.
Alisema mkuu huyo wa wilaya ya Bukombe ndiye anayemfanya aone wakuu wa wilaya walioteuliwa kutoka upinzani ni watatu na nusu kwa kuwa alikaa muda mfupi Chadema kabla ya kurudi CCM.
Rais alisema lengo lake ni kujenga nchi yenye umoja, isiyo na ubaguzi wa dini, kabila wala vyama na yuko tayari kuwashirikisha wote wanaotaka kupeleka mbele nchi.
“Ndiyo maana niliweza kumchagua Profesa Mkumbo alikuwa ACT, akawa katibu mkuu Wizara ya Maji. Lakini waliomsababisha ni CCM,” alisema.
Dar es Salaam kuna wapigaji
Kuhusu utendaji wa wakuu wa mikoa, Rais aliusifu Dodoma kwa kuongoza kwa ukusanyaji mapato, ikiwa ni siku chache baada ya kupandishwa hadhi na kuwa jiji.
“Dodoma inaogoza kwa makusanyo mengi, Sh24.5 bilioni. Sasa unaweza kujiuliza, Dodoma kuna nini?" alisema Rais.
"Yule mkuu wa mkoa wa Dodoma, RAS (katibu tawala), mstahiki meya na wananchi wa Dodoma wana genes za namna gani ukilinganisha na Dar es Salaam ambayo ina population (idadi) ya watu 5.5 milioni?”
Alisema mkoa wa Dar es Salaam uliwekewa malengo ya kukusanya Sh12 bilioni lakini hauklufikisha.
“Sasa unaweza ukajua kwamba hapa Dar es Salaam kuna upigaji tena wa nguvu. Lakini viongozi wapo."
Pia alisema hata wilaya ya Kinondoni ambaye aliyekuwa akiiongoza, Ali Hapi amempandisha cheo na kuwa mkuu wa mkoa, ilikuwa ya mwisho.
"Sasa nikawa najiuliza sijui nimtumbue hapa hapa au," alisema Rais Magufuli huku akikuna kichwa.
"Kweli wala sifichi, nikasema wilaya ilikuwa ya upinzani ile. Lakini hivi vitu vinatia aibu."
Huku akizungumzia majiji mengine, alikosoa pia jiji la Mbeya akisema limeshika nafasi ya mwisho kati ya majiji sita nchini.
“Yaani jiji nililotangaza miezi miwili mitatu iliyopita ndio linaongoza! Nimejiuliza sana, labda tuweke mikakati ya kufanya; jiji linaloshindwa kukusanya linashushwa chini. Utaitwaje jiji wakati hata hujui kukusanya?” alihoji.
Alizitaja pia halmashauri za Mbulu na Mbinga akisema zimekuwa za mwisho katika ukusanyaji wa mapato, huku akiwataka wakuu wa mikoa kusimamia kazi hiyo.
“Wakuu wa mikoa ni kila kitu, hakuna mahali popote panaweza kukukwamisha. You are everything," alisema.
"Sasa mimi huku Rais ninakazania mapato huku, wewe rais wa mkoa ule unashindwa kusimamia mapato, kwa nini nisijiulize kwamba hufai?
"Survival ya nchi hii ni mapato, fedha zinazokusanywa ziende kwenye miradi ya maendeleo ili nchi iende mbele. Hapa Dar es Salaam, wala siyo siri, wakikutana kwenye vikao, madiwani kama wamekaa siku moja wanalipana siku nne. Kila mmoja anajua. Wakikutana siku mbili zitakazojazwa pale ni siku nne. PCCB wapo. Unategemea utapata hela gani kwa maendeleo?”
Alisema kutokana na hali hiyo kero za wananchi wakiwemo wafanyabiashara ndogo hukosa nafasi za kufanya biashara licha ya kuwepo kwa viongozi.
Ugumu wa kazi
Akizungumzia majukumu ya uongozi alisema kazi ya urais ni ngumu na kuwashauri viongozi kupambana na ugumu huo wa kazi.
“Ndugu zangu, hizi kazi sisi zote tumepewa dhamana. Hakuna mwenye guarantee (uhakika) ya kazi hii. Hata mimi wala sina guarantee ya kazi hii kwamba I will be a permanent president, No (nitakuwa rais wa kudumu, hapana),” alisema.
“Kazi ya kukaa usiku kucha siku nyingine hulali, mafaili yanakuja yanataka utoe solution, it’s a terrible job (ni kazi ya ajabu). Mengine yapo kwenye kitanda mafaili, nilimpeleka mtu nikambia huu ndiyo urais, ningejua nisingeuomba.”
Miongoni mwa viongozi walioapishwa ni pamoja na Brigedia Jenerali Nicodemus Mwagela kuwa mkuu wa Mkoa wa Songwe akichukua nafasi ya Chiku Galawa aliyesataafu.
Mwingine ni Brigadia Jenerali Marco Gaguti kuwa RC Kagera akochukua nafasi ya Meja Jenerali Salum Kijuu aliyestaafu.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa wikaya ya Kinodoni Ally Hapi- Iringa, Albert Chalamila RC Mbeya.
Makatibu wakuu waliopishwa ni pamoja na Joseph Mchweshaija amayekwenda Wizara ya Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Andrew Massawe kuwa Katibu mkuu katika Ofisini ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu wa Bunge, wazee na walemavu.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa wikaya ya Kinodoni Ally Hapi- Iringa, Albert Chalamila RC Mbeya.
Makatibu wakuu waliopishwa ni pamoja na Joseph Mchweshaija amayekwenda Wizara ya Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Andrew Massawe kuwa Katibu mkuu katika Ofisini ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu wa Bunge, wazee na walemavu.
Makatibu tawala walioapishwa ni Eric Shitindi- Njombe -Mwaduka Kessy -Dodoma, Jill Maleko- Mtwara, Abubakari Kunege- Dar es Salaam, Happiness Senada- Iringa.
Wengine ni Carolina Mfakula- Mara, David Kafulila- Songwe, Dennis Isdory- Geita, Abdallah Malela- Katavi, Rashid Mchata-Kigoma, Misaile Musa-Manyara,
Christopher Kadio- Mwanza and Riziki Shemdoe- Ruvuma.
Wengine walioapishwa ni manaibu Katibu wakuu ambao ni pamoja na Dk Jim Yonazi anayekwenda Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na usafirishaji na Edwin Mhede anayekwenda Wizara ya Viwanda na Biashara.
Wengine ni Carolina Mfakula- Mara, David Kafulila- Songwe, Dennis Isdory- Geita, Abdallah Malela- Katavi, Rashid Mchata-Kigoma, Misaile Musa-Manyara,
Christopher Kadio- Mwanza and Riziki Shemdoe- Ruvuma.
Wengine walioapishwa ni manaibu Katibu wakuu ambao ni pamoja na Dk Jim Yonazi anayekwenda Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na usafirishaji na Edwin Mhede anayekwenda Wizara ya Viwanda na Biashara.
Comments
Post a Comment