NEWS: Salamba wa Uturuki ndiyo kama mlivyosikia

Kartepe, Uturuki. Mshambuliaji mpya wa Simba, Mohammed Salamba amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao mbele ya kocha Mbelgiji Patrick Aussems jambo linalomfanya ajione mwenye bahati.
Salamba alifunga bao hilo dakika ya 61, dhidi ya klabu ya Mouloudia Oujda FC ya Moroccco katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa The Green Park ndani ya mji wa Kartepe, Uturuki.
Salamba alisema: "Anashukuru Mungu kufunga bao hilo kwani si yeye peke yangu ni kutokana na ushirikiano na wenzake kikubwa ni kupambana."
Amesema, bao alilofunga limemwongezea nguvu na hali ya kujiamini ndani ya kikosi hicho chenye ushindani mkubwa wa namba.
"Kwangu imenisaidia kwa sababu nimepata nguvu ya ziada na hali ya kujiamini kama unavyojua ugeni pamoja na ushindani mkubwa wa namba,"alisema Salamba ambaye amesajiliwa na Simba akitokea Lipuli FC ya Iringa.
Akizungumzia nafasi yake ya kucheza kikosi cha kwanza, Salamba amesema: "Hiyo ni kazi ya mwalimu maana mimi ninachotakiwa kufanya ni kupambana tu uwanjani ili mambo yaende."
Comments
Post a Comment