NEWS: Simba kuliamsha na Ittihad ya Morocco


By Doris Maliyaga
Kartepe, Uturuki. Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba kesho Ijumaa watakuwa uwanjani kucheza na Ittihad Riadi de Tanger ya Morocco kwenye Uwanja wa The Green Park, Uturuki.
Simba itacheza mchezo huo ambao utakuwa ni wa pili baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mouloudia Oujda pia ya Morocco mechi iliyovunjika baada ya mvua kubwa kunyesha.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kwao utakuwa mchezo mzuri baada ya ule wa kwanza.



"Itakuwa mchezo mzuri kwangu kujua zaidi ni aina gani ya wachezaji nilionao,"alisema Ausemms.
Mbali na mchezo huo, Simba inatarajia kucheza mchezo mwingine wa tatu kabla kurudi Tanzania.

Comments