SPORT NEWS: Mshahara wamkimbiza Vidal Bayern Munich

Arturo Vidal ametoka Bayern Munich kwa Barcelona. Reuters
Ubahiri uliokithiri kwenye Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ndiyo sababu iliyomfanya kiungo wake Arturo Vidal kukimbilia Barcelona ya Hispania.
Vidal mwenye miaka 31 amejiunga na Barcelona kwa ada inayosemwa Euro 25 milioni, ingawa haijabainishwa mshahara atakaolipwa akiwa Camp Nou.
Mchezaji huyo aliwaambia rafiki zake kuwa asingehama Munich aliyojiunga nayo mwaka 2015 kama angekuwa analipwa vizuri.
Barcelona ilitangaza jana kuwa mchezaji huyo alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kumwaga wino kuitumikia klabu hiyo.
Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde, amesema ujio wa mchezaji huyo utaiongezea nguvu kampeni yao ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England na kupigania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Vidal, raia wa Chile alikuwa akihusishwa na kujiunga na timu kadhaa kabla ya kuichagua Barca, ambako amesema ataitumikia hadi atakapoamua kwenda kumalizia soka kwenye klabu iliyomkuza ya Colo-Colo ya nyumbani kwao.
Comments
Post a Comment