SPORT NEWS: Zahera aangalia mambo matatu Yanga, Mawenzi Market






Morogoro: Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema katika mchezo wa kesho wa kirafiki dhidi ya Mawenzi Market ataangalia mambo matatu tu kwa wachezaji wake kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kocha Zahera amesema mambo ambayo anataka kuyapima kesho ni kuangalia kiwango cha fiziki ya wachezaji wake jambo la pili analotaka kuliangalia ni uwezo wa kucheza kitimu kwa mfumo watakaoutumia pamoja na kuangalia nidhamu ya mchezaji mmoja mmoja jinsi wanavyoshika maelekezo yake atakayowapa kabla ya kuingia uwanjani.
Zahera amesema wakiwa kambini Mkoani Morogoro wachezaji wake wamekuwa na wakati mzuri wa kufanya mazoezi ya kutosha ukilinganisha na walivyokuwa jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo amesema wakiwa hapa wamekuwa na vipindi vya kutosha vya mazoezi ambavyo sasa vinaweza kuzilinganisha na timu za Simba na Azam zilizoweka kambi nchini Uturuki na Uganda.
Amesema ingawa kazi kubwa imefanyika, lakini bado kikosi chake hakijafikia ubora anaoutaka.
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea Kilosa itacheza mechi ya mwisho mkoani hapa Jumatatu dhidi ya kombani ya wilaya hiyo.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh Amesema mchezo huo ni maalum kwa mashabiki wa timu hiyo waliopo Kilosa kuiona timu yao.
Amesema hata hivyo bado uongozi wao unalifanyia kazi ombi la kocha mkuu Mwinyi Zahera aliyetaka kitafutiwa mechi ngumu zaidi baada ya mechi hizo.

Comments

Popular Posts