NEWS: Diwani wa 54 Chadema ajiunga CCM

Dodoma. Diwani wa kata ya Kizota (Chadema) mkoani Dodoma, Jamal Ngalya amejizulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini na kujiunga na CCM.
Ngalya ametangaza uamuzi wake huo leo Jumatano Agosti Mosi, 2018 mjini hapa katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Ngalya ambaye alichaguliwa kuwa katibu wa madiwani wa chama hicho mkoani hapa, amesema anarejea CCM kwa kuwa waliomkata jina lake katika kura ya maoni kwa sasa hawapo madarakani.
Amesema amechukua uamuzi huo bila kushawishiwa na mtu ili kuungana na timu ya Rais John Magufuli.
Soma Zaidi:
Aliyekuwa diwani wa kata ya Nkuyu wilayani Kyela mkoani Mbeya, Kaini Mwakaniemba alikuwa diwani wa 53 wa Chadema kujiunga na CCM. Alitangaza uamuzi wake huo juzi Julai 30, 2018.
Siku chache kabla ya Nkuyu kutangaza uamuzi wake huo, aliyekuwa diwani wa Chadema kata ya Nsalanga mjini Mbeya, Mchungaji David Ngogo alitangaza kujiuzulu na kujiunga na CCM.
Comments
Post a Comment